Thursday, February 26, 2015

ZAIDI YA WAKUFUNZI (30) MKOANI MBEYA WASHIRIKI KATIKA SEMINA YA M-PAWA

Zaidi ya wakufunzi (30) wa Wilaya ya Mbozi Mkoa wa Mbeya washiriki katika semina ya elimu ya kifedha na huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha zaidi ya wakulima 140,000 Tanzania. Semina hiyo iliandaliwa na Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) na Shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe chini ya udhamini wa (USAID).
Mshauri wa biashara wa shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe, Reginald Mpolo akitoa elimu kwa wakufunzi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya (hawapo pichani) wakati wa semina iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na Benki ya Afrika (CBA) hapo jana juu ya huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha wakulima 140,000 Tanzania kupata Elimu ya M-Pawa na elimu ya kifedha. Semina hiyo ilidhaminiwa na (USAID).
Baadhi ya wakufunzi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wakimsikiliza Mshauri wa Biashara wa shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe, Reginald Mpolo akitoa elimu wakati wa semina hiyo hapo jana iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na Benki ya Biashara ya Afrika (CBA) juu ya huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha wakulima 140,000 Tanzania kupata Elimu ya M-Pawa na elimu ya kifedha. Semina hiyo ilidhaminiwa na (USAID).
Baadhi ya wakufunzi wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na wa shirika lisilo la kiserikali la TechnoServe wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya semina kumalizika hapo jana iliyoandaliwa na Vodacom Tanzania na Benki ya Afrika (CBA) iliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya kifedha na huduma ya M-Pawa inayolenga kuwanufaisha wakulima 140,000 Tanzania. Semina hiyo ilidhaminiwa na(USAID).

No comments: