Monday, May 25, 2015

TPSC yazindua jengo jipya jijini Mbeya

Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani wa tano kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa serikali  Mkoa wa Mbeya na TPSC baada ya uzinduzi wa jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya, wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa TPSC tawi la Singida, Dkt. Enortha Shayo, Makamo Mkuu wa TPSC, Dkt Henry Mambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Jiji la Mbeya Musa Zungira na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapuga wa pili kulia ni Mkuu wa TPSC Said Hamis Nassor na wa kwanza kulia  ni Mkurugenzi wa TPSC tawi la Mbeya Augustino Mhina.Picha na www.inocomm.blogspot.com
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akimsikiliza Mkuu wa TPSC Tanzania, Said Hamis Nassor, baada ya kuzindua jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya,wengine wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa TPSC tawi la Mbeya Augustino Mhina.
Sehemu ya wafanyakazi na wanafunzi wa TPSC tawi la Mbeya wakimsikiliza Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akizungumza na watumishi wa TPSC tawi la Mbeya,katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Nyerembe Munassa.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akipata maelezo kutoka Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la MbeyaMusa Zungira, kuhusu  jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya eneo la Soko Matola, wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo cha utumishi wa Umma Tanzania, Said Hamis Nassor wa pili kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Athanas Kapunga .  
Waziri akipata maelezo ya jengo hilo kutoka kwa watendaji wa Manispaa ya Mbeya na TPSC.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akikata utepe kuzindua jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya eneo la Soko Matola, jijini hapa, kulia ni Mkuu wa TPSC Said Hamis Nassor na kushoto ni Meya wa Jiji la Mbeya, Athanas Kapunga.
Waziri wa  Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani akishusha pazia kuashiria uzinduzi wa jengo jipya litakalotumiwa na TPSC tawi la Mbeya eneo la Soko Matola, kulia ni Musa Zungira,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.   

No comments: