Wednesday, July 8, 2015

HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI NCHINI

CH10 NEWS
CCM,yasema haina kanuni wala utaratibu wa wagombea kukata rufaa endapo hawatateuliwa uraisi na kudai hakifanyi kazi kwa presha za mtu. http://youtu.be/E-gultoau9E
 Serikali yaahaidi kupunguza tatizo la miundombinu mashuleni sambamba na kuwataka wazazi na walimu kushirikiana kwa pamoja ili kuboresha elimu. http://youtu.be/KRcCVytPv6I
 Wananchi mbalimbali wamejitokeza katika Maonyesho ya Kimataifa ya biashara ya Sabasaba huku wakitaka uongozi wa maonyesho hayo kuyaboresha zaidi. http://youtu.be/qieHz2XE2-k
 Mikoa ya kanda ya ziwa inategemea kunufaika na mradi wa ujenzi wa hospitali ya kansa itakayo jengwa mkoani Kagera kwa msaada wa kampuni ya VIP Engeneering. http://youtu.be/Y9EmxokCfmw
 Katika kukabiliana na ongezeko la wagonjwa na uhababa wa majengo katika hospitali ya KCMC, ujenzi na upanuzi wa majengo hospitalini hapo waanza. http://youtu.be/BxqO5A25mzE
 Serikali yaombwa kongeza bajeti ya wizara ya maendeleo ya jamii ili kuiwezesha wizara hiyo kutimiza majukum yake kwa ukamilifu. http://youtu.be/diHBJCA2GoQ
 Wananchi wa Bariadi Mkoani Simiyu wapata taharuki baada ya kukuta kaburi la merehemu kikiwa limekewa vifaa mbalimbali juu yake. http://youtu.be/-ygrXdQ5LbU
 TBC NEWS
Raisi Jakaya Kikwete afungua zoezi la uandikishaji BVR mkoani Pwani huku akitoa wito kwa watanzania kujitokeza kujiandikisha.https://youtu.be/y6lC3MLU5js
 Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party Christopher Mtikila ataka uchaguzi mkuu kuwa huru na wa haki huku akiapa kuwashitaki mahakamani wale wote waliokiuka sheria za uchaguzi. http://youtu.be/5G8haiXEKjU
 Wizara ya mali asili na utalii yasema kumekuwa na ongezeko la utalii wa ndani kufuatia kampeni mbalimbali za uhamasishaji wa kutembelea hifadhi hizo. http://youtu.be/YQTkSs0zdhw
 Vurumai zazuka katika zoezi la uandikishaji BVR mkoani Morogoro huku afisa Mtendaji akinusurika kipigo baada ya kuingilia utaratibu uliowekwa na wananchi. http://youtu.be/mhouAJ5jIWM
 Mkuu wa jeshi la polisi nchini asema matukio ya makubwa ya uhalifu mkoani Tabora yanatokana na wimbi kubwa la wahamiaji haramu wanao ingia na silaha nchini. http://youtu.be/DAHdcLe4GQk
 Mbio za mwenge zaendelea kwa siku ya 6 mkoani Mbeya, huku uongozi wa mbio hizo ukitoa rai ya kujengwa kiwanda cha kakao ili kuwanuifaisha wakulima. http://youtu.be/9N8oqm8sWi4
 Azam news
Joto la uraisi linaendelea kupanda ndani ya CCM mkoani Dodoma baada mchakato wa kumpata mgombea uraisi kuanza.http://youtu.be/bIV9p4q9Brk
 Kundi la kigaidi la Alshabab lawaua watu 14 na kujeruhi wengine kadhaa nchini Kenya karibu na kambi ya kijeshi.http://youtu.be/nAg9bpjOMhQ
 Utafiti uliofanywa hivi karibuni waonyesha asilimia 70 za magonjwa yawapatayo binandamu huambukizwa toka kwa wanayama wa kufuga . http://youtu.be/pU7VpXdO0g4
 Katibu wa itikadi na uenezi wa Chaadema akosoa hukumu iliyotelwa kwa mawaziri wa zamani Daniel Yona na Basil Mramba.https://youtu.be/kgjOPY2u9yA
 Star tv news
 Chadema mkoani Tabora chawataka wanawake kuacha uoga ambao umewafanya wawe na maisha magumu kuwania uongozi.http://youtu.be/UKIwBB_YzXA
 CCM mkoani Mwanza yawaasa wananchi kutofanya makosa kwa kuchagua wawakilishi wasio na msaada katika maendeleo ya maeneo yao. http://youtu.be/2KxsUiHo1uY
 Madiwani wa halmashauri ya Geita waitupia lawama halmashauri hiyo kwa kushindwa kutekeleza maamuzi waliyokubaliana juu ya upungufu wa walimu katika shule za vijijini. http://youtu.be/P6xGTI72iSM
 Viongozi wa dini wawataka watangaza nia watakao kosa nafasi kukubali matokeo ili kudumisha amani na mshikamano katika vyama vyao na taifa kwa ujumla. http://youtu.be/fHEhDkak7yI

No comments: