Monday, July 6, 2015

IJUE SAYANSI YA MOTO NA JINSI YA KUKABILIANA NAO 2.

 Na Nasibu Mgosso
Awali ya yote nichukue fursa hii kuomba radhi kwa makosa ya kiuandishi yaliyo jitokeza katika makala iliyopita  ambayo  mwanzoni  mwa paragrafu  ya kwanza nilianza kueleza moto nikitugani,  lakini katika maelezo kulitokea mkanganyiko,  Sehemu hiyo ilipaswa isomeke hivi:

Moto ni mgongano endelevu  wa  kikemikali ambao huzaa joto na mwanga.  Mgongano  huo  endelevu   utasababisha muwako  ambao  utaendelea   kukua  endapo  utapata  vitu vikuu  vitatu  ambavyo  ni joto,  hewa  ya  oksijeni  na kuni(vitu  vinavyoungua).   Vituhivyo  kitaalam  tunaviita  ’fire element’.
Oksijeni nimiongoni mwa  vitu vinavyo  saidio moto kuwaka  haizalishwi na moto kamailivyo someka  katika  makala iliyo pita.
Baada ya marekebisho hayo  sasa tuendelee na  kinga na taadhari dhidi  ya moto.
Kunavyanzo vingi vya moto  lakini chanzo kikubwa ni  sisi  Binadamu  kwa sababu  ya asili na alakati za maisha ya kila siku  kuhusisha matumizi ya moto kwa   maana ya mwako,  nishati ya umeme pamoja na vyombo vya usafiri na usafirishaji.  Katika mahitaji hayo inatulazimu kujenga urafiki na moto bila kujali hatari iliyopo.
Aina ubishi kwamba moto ni nyenzo muhimu katika  maisha yetu ya kila siku,   na niadui yetu mkubwa  sana anaye penda kutu shambulia  akitokea ndani ya jengo au chombo .  
 Kutokana na mbinu hiyo , moto  umekuwa ukisababisha  ualibifu wa mali, ulemavu,  pamoja na vifo kila siku iendayo kwa mungu.
Hatuwezi kuepuka isitokee kabisa lakini tunaweza kupunguza  matukio hayo kama tutapata elimu sahihi ya kinga na taadhali  ya moto.

KINGA NA TAHADHARI KATIKA MAJENGO.
Tuki zingatia kanuni za ujenzi wa majengo  na kuwatumia  wataalamu  kwakufuata ushauri wao na kuheshimu taaluma zao tunaweza kufanikiwa kupunguza majanga ya moto pamoja na majanga mengine.
Nianze na  umeme kama miongoni mwa  chanzo cha moto katika maeneo ya mijini  japokuwa kwasasa vijijini nako huduma hiyo imeanza kupatikana.  Nivyema kutumia  mafundi umeme walio somea na kusajiliwa na mamlaka husika.
Epuka kutumia   vifaa visivyo na ubora   vinavyo patikana kwa bei ya chini,  kumbuka bure ghali . Matumizi ya vifaa vya umeme  chakavu  kama jiko, pasi,  jokofu,  Oveni   kutoka nje , siyo salama kwasababu vinakuwa vimechoka  hivyo  vinaweza kusababisha  hitilafu na kusababisha moto.
Matumizi  ya vifaa vingi katika  chanzo kimoja(extension ) vinaweza kusababisha moto kutokea ,  ni vizuri unap weka  mfumo wa umeme  katika jengo weka swichi soketi zaidi ya moja  katika kila chumba kulingana na ukubwa pamoja na  mahitaji.  Kwa mfano  sehemu ya kupumzikia(seating room ) ni vema ikawa na vyanzo vingi vya umeme   kwa sababu  matumizi  uwa makubwa ukilinganisha na  vyumbani.
Aitha  mfumo wa umeme ukaguliwe marakwa mara kuangalia kama kuna hitilafu,  badirisha waya kila baada ya miaka 15. Hakikisha waya wa ethi hauna tatizo lolote pia  shaba inayo chimbiwa aridhini iwe na ukubwa wa kutosho  kulingana na mahitaji ya jengo.
Kwa maeneo ya mikoa yenye  Radi kwawkiasi kikubwa,  vifaa vya  mawasiliano kama  minara na setelaiti dishi  nivizuri viwe  na mfumo wa ethi wa kujitegemea  kwasababu  uwezekano wa kupigwa na  radi   na kusababisha moto  nimkubwa  zaidi.
Jinsi ya kutambua kama mfumo wa  ethi haufanyi kazi.
  Kama mfumo wa  ethi haufanyi kazi  vizuri  mambo yafuatayo yatajitokeza,   vifaa vya ndani kama friji vitakuwa na  shoti   ukigusa utahisi hali ya  kutetemeshwa ,   jua kwamba  umeme una rudishwa kwenye soketi  bleaka  ili upelekwe aridhini  kupitia mfumo wa  ethi  lakini  kwasababu mfumo huo haufanyi kazi, umeme unakosa muelekeo na kurudi katika mzunguko,   ikiwa kuna  sehemu yenye hitilafu  moto utaanzia apo,  fanya  marekebisho   kabla  ajari  haijatokea.
Matumizi ya mishumaa  bila ya taadhari ni hatari sana,  imekuwa kawaida kusikia  nyumba imeungua  chanzo kikiwa  mshuma .   Kama  ni lazima   kutumia mshumaa  chukua hatua zifuatazo ,  chomeka  mshumaa katika mdomo wa chupa  sio plastiki ,  tumia nguvu kuushindilia, hakikisha kiasi  kisicho pungua nusu kidole kimezama ndani ya chupa.
Weka  mbali na ukuta, pazia, kitanda, viti na vitu vyote vinavyo weza kuungua.  Nihatari kulala  ukiwa umeacha mshumaa unawaka,   usiweke vimiminika vinavyo lipuka ndani . Vyombo kama Pikipiki na jenereta  ni hatari kuhifadhiwa ndani  pia mafuta ya akiba kwamatumizi ya vyombo hivyo yasi hifadhiwe ndani .
Matumizi  ya gesi  ya zingatie usalama kulingana na maelekezo  ya kitaalamu, watoto wa dogo wasitumie  wakiwa pekeyao.
Zima vifaa vya umeme kama havitumiki au kama hakuna mtu nyumbani.  Weka  ving’amuzi  vya moshi au joto katika nyumba yako , kuwa na mitungi ya kuzimia moto ya huduma ya kwanza hakikisha familia ina jua jinsi ya kuutumia.
Kumbuka king’amuzi cha joto au moshi hakizimi moto  kita piga alam kuashilia tukio,  wewe utatakiwa kuzima umeme  wa nyumba yote   kagua   kujua  kama kuna  tukio.  Ikiwa utabaini moto  tumia mtungi  wako kuukabili mapema kabla haujawa mkubwa,  fahamu mtungi huo ni wa huduma ya kwanza,  hauwezi kuzima moto mkubwa.
Pia vipo vifaa kama hivyo  vinavyo fanya kazi bila kutegemea uwepo wa mtu,  vina ji ongoza vyenyewe vinatumia  mfumo wa kung’amua joto na likizidi asilimia 68 chupa itapasuka ambapo ita ruhusu mgandamizo wa hewa  yenye mchanganyiko na dry powder  kutoka na kupunguza kiwango cha okisijeni ili kuzimamoto.  Faida za kifaa hiki ni kubwa  kwasababu  kitaokoa hatakama nyumbani au ndani ya jengo hakuna mtu.
Aidha  majengo marefu zaidi ya ghorofa 7 yafungwe mfumo wa kuzima moto wenye  kujiongoza wenyewe unao tumia maji, (automatic sprinkler  system ) na yawe na mabomba  yasiyo na maji yaliyo anzia chini ya jengo kwa nje  yatakayo tumiwa na zimamoto kupandisha maji juu pindi moto unapo tokea.
Sambamba na yote hayo kumbuka kuomba msada,  pigakelele kuita watu,  wasiliana na Jeshi la Zimamoto na  Uokoaji  kwa simu namba 114 eleza hali halisi ya tukio, eneo husika  na  jinsi ya kufika  hapo.
Angalizo, 114 ni namba ya dharura kwajili ya matukio ya dharura ambayo haya husiani na  uvunjaji  wa sheria,   namba hihi inapatikana kwa mitandao yote katika mikoa yote Tanzania Bara,   matumizi  mabaya ya namba hihi ni matumizi mabaya ya mitandao,  kuwa makini  Fahamu kuwa miongoni  mwa  sababu zinazo  sababisha Zimamoto  kuchelewa  katika matukio  ni taarifa za matukio zisizo za kweli  za mara kwa mara. Inapo tokea kuna tukio la kweli inachukua muda  mrefu kubaini ukweli  huo  na hiyo nimoja ya sababu za wao kuchelewa kufika eneo la tukio.
Tukishirikiana  kwapamoja tuta punguza majanga ya moto.
Kwa maoni , ushauri tuwasiliane kwa

                                                                nmgosso@yahoo.com / godfreypeter37@yahoo.com

     




No comments: