Monday, August 31, 2015

WALIMU ARUSHA WAIDAI SERIKALI BILIONI 4

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha ,Mwalimu Jovin  Kuyenga akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisini kwake  juu ya deni la shilingi bilioni 4 wanalodai  kwa serikali, kushoto ni Katibu wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan Saidi.

Na Woinde Shizza,Arusha
CHAMA cha Walimu mkoa wa Arusha CWT wamelalamikia serikali na kuitaka kutekeleza kwa wakati madeni yao la zaidi ya billioni 4 kwani yamekuwa kikwazo katika ufanisi wa kazi hali ambayo inapelekea walimu wengi kushindwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kujituma jambo ambalo linaweza kushusha kiwango cha elimu nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa waArusha Mwalimu Juvin Kuyenga amesema, kumekuwa na  chanagamoto kubwa ambazo zinakwamisha ufanisi wa kazi kwa walimu kwani wanazidai halmashauri zilizopo mkoani zarusha zaidi ya billioni nne ,amabapo katika jiji la arusha wanadai millioni  987,689,00,Arumeru billioni
2,996,607,848.21,Karatu  millioni 423,983,820,Longido millioni 171,112,680,
Ngorongoro million 169,000,000, na Monduli 135,832,000.

Mwalimu Kuyenga ameendelea kusema kuwa,madeni haya yanatokana na madai mbalimbali ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara
,mafunzo,uhamisho,matibabu na likizo pamoja na mapunjo ya mshahara na
madeni haya yamekuwa ni kero kubwa  na kusababisha wakati mwingine walimu kuzichukia kazi zao.

Alisema kuwa Walimu wamekuwa wakigota madaraja bila kupanda kwa muda mrefu kati ya walimu 12,319 waliopo mkoani arusha walimu 5,364 wamegota kwenye madaraja yao na bado hawajafunguliwa  pamoja na serikali ilishatoa waraka wa kufungua madaraja tangu julai 2014 hivyo wametaka seriakali kuhakikisha inapandisha madaraja kwa wakati.

‘Posho ya madaraka kwa viongozi wa elimu, wakuu wa shule,wakuu wa vyuo
kutokana na waraka wa seriakali uliotolewa mwaka jana posho hiyo alitakiwa ianze kutolewa kuanzia julai mwaka huu 2015 lakini hadi sasa bado pesa hiyo haijanza kutolewa hii inakuwa kama danganya toto kwa viongozi wetu” alisema mwalimu Juvin Kuyenga.

Hivyo  wameilalamikia serikali juu ya kuchelewesha kwa malipo kwa wastaafu, sababu kuna walimuwaliostaafu toka january  zaidi ya walimu 67 huku wakiishi katika mateso ilihali wameshastaafu kazi na mpaka leo hawajapata viiinua mgongo vyao

“Tunaidai serikali sababu tunapowasiliana na hawa wa mifuko ya hifadhi za
jamii inasema serikali bado haijawarejesha michango ya walimu inayotakiwa kupelekwa hivyo na danadana hizi zinawafanya walimu kuona haki zao zinanyonywa kwani utasababisha ufanisi kuwa mdogo makazini” Alisema

Sababui swala hili laweza kupelekea malumbano kati ya walimu na serikali
ukizingatia katika kipindi cha kueleka katika uchaguzi ,mitihani ya darasa
la saba na kidato cha nne kwani kukataa huku tamaa kunaweza kupelekea vitu hivyo vya taifa kushindwa kufanikiwa.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan Saidi amesema chama hicho kimetoa wiki mbili kwa  waajiri wa halmashauri zilizopo mkoa wa arusha kuwarudisha majumbani walimu waliostaafu na wanaostaafu na wasipofanya hivyo watawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwashtaki mahakamani kwani wamekuwa wakiteseka sana baada ya kustaafu na ni kinyume cha sheria .

Mwalimu Saidi , amewataka wagombea wa Uraisi kutazama vipaumbele vya walimu walivyovitoa likiwemo la kuwapatia walimu  kompyuta mpakato (laptop)  wakati wanamahitaji mengi na ya  msingi zaidi ya hayo ikiwa ni pamoja na mishahara isiyokidhi mahitaji ya walimu na kurejeshwa na kwa posho ya kufundishia kwa walimu.

Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa vyanzo vyetu kuwa baraza la kuu la
walimu tanzania  wanatarajiwa kukutani mkoani dodoma  Agosti  31 hadi
Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya kutoa matamko ya kitaifa juu ya kero hizi nyingi wanazozipata walimu.

No comments: