Wednesday, November 25, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

Serikali imetangaza kusitisha sherehe ya maazimisho ya siku ya ukimwi duniani badala yake pesa za sherehe hizo zitumike kununulia dawa; https://youtu.be/hUPjDKtZyjs

Mkuu wa wilaya ya Babati ameagiza kukamwatwa mara moja kwa hakimu wa mahakama ya mwanzo,afisa mtendaji pamoja na mwenyekiti wa kitongoji kwa tuhuma za kudhulumu ardhi; https://youtu.be/dvMgfiN4g7g

Serikali imesema haitogharamia uendeshaji wa vikao kwa watendaji wake badala yake watumie TEHAMA kuendesha vikao hivyo lengo likiwa ni kupunguza gharama;https://youtu.be/Fa_05inCsso

Jamii nchini imeshauriwa kuwa karibu na watoto wao ili kubaini changamoto zao juu ya unyanyasaji wa kijinsia na kuzitafutia ufumbuzi kwa wakati;https://youtu.be/cyGkL7GJ_mI

Mamlaka ya bandari nchini TPA imewataka mawakala wa forodha kutumia mfumo kielektroniki katika kuwasilisha nakala mbali mbali; https://youtu.be/OVGBXpMrVBw

Barala la taifa la uwezeshaji wa wananchi kiuchumi NEEC limesema litabdili sera yake ya mwaka 2004 kwa lengo la kuzingatia masuala ya kijinsia;https://youtu.be/3TlIG5OAsps

Klabu ya Simba imekanusha tuhuma zilikuwa zimeenea ya kwamba imeutelekeza uwanja wake ulipo maeneo ya Bunju jijini Dar es Salaam;https://youtu.be/XQYyOCjykGQ

Wafuasi wa CCM wilayani Ulanga wachomewa nyumba zao mara baada ya kutangazwa kwa  matokeo ya uchaguzi wilayani humo; https://youtu.be/xtvKIzKzt3A

Mahakama kuu ya Mwanza inatarajiwa kutoa hukumu kesho kuhusu kesi ya madai ya zuio la kuuaga mwili wa marehemu Alphonce Mawazo; https://youtu.be/N48e9xm8ZII

Imeelezwa kuwa wazee wengi nchini bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha hususani wale wanaoishi maeneo ya vijijini.https://youtu.be/UdNBXaZ5STY

Mamlaka ya usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA mkoani Tabora imeshauriwa kubadili mfumo wa ukataji wa tiketi ili kuondoa usumbufu waupatao abiria;https://youtu.be/3kPvhWOEvLg

Wataalamu wa mifugo kutoka nchi mbalimbali za Afrika wamekutana jijini Tanga kujadili namna ya kuongeza uzalishaji wa maziwa na bidhaa nyingine zitokanazo na maziwa; https://youtu.be/aupWgyw9V3o

Klabu ya Geita Gold sports ya mkoani Geita imempa mkataba wa mwaka mmoja kocha wa zamani wa klabu ya Simba Suleiman Matola; https://youtu.be/QxQiMsnmgfA

Shirikisho la soka duniani FIFA kwa kushirikiana na chama cha mpira wa miguu wa wanawake Tanzania TWFA limeandaa tamasha maalum kwa lengo la kuhamasisha soka la wanawake nchini; https://youtu.be/YXoSdZm_-RE

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe.Paul Makonda awatupa rumande watendaji wa ardhi baada ya kuchelewa kufika kwenye eneo la kazi; https://youtu.be/Isvg99XFZAY

Rais John Magufuli afuta sherehe za maadhimisho ya siku ya ukimwi na kuagiza fedha zilizotengwa zitumike kununulia dawa na vitendea kazi. https://youtu.be/b2HjW-K3FPE

Uchafu waelezwa kukithiri katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam licha ya agizo lililotolewa na Rais Magufuli hivi karibuni. https://youtu.be/P2Z35Berges

Jaji mkuu Mohammed Chande awataka wanahabari watoao habari za mahakamani kuzingatia umakini,weledi,maadili na taratibu za kimahakama wakati wanapo andika habari hizo. https://youtu.be/h0p9wif7gVU

Ukatili wa kijinsia waelezwa kuwa tatizo kubwa nchini ambalo hupelekea athari mbalimbali kama vile mimba za utotoni, maambukizi ya ukimwi na kuminya haki za msingi za binadamu. https://youtu.be/TdGTQiAi4Fg

Shirika la haki elimu limezindua jopo la washauri mabingwa wa elimu nchini ikiwa ni jitihada zake za kuboresha shughuli za utafiti,uchambuzi wa sera na utetezi katika sekta ya elimu. https://youtu.be/Z3Dz_ggokg8

Kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KIA) kimeanza kufanyiwa ukarabati mkubwa katika njia za kuingia na kuruka ndege kufuatia msaada uliotelewa na nchi ya Uholanzi.https://youtu.be/DZUxaAfeFgg

Jukwaa huru la wazalendo limewapongeza wabunge Zitto Kabwe na mbunge wa Singida magharibi kwa Elbariki Kingu kwa kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kukataa posho za vikao vya bunge. https://youtu.be/GG2Ej3FD03E

Mvutano wa wabunge juu ya mkopo wa magari wa milioni 90 waripotiwa kuendelea huku baadhi yao wakiridhia na wengine wakilalama. https://youtu.be/Gus65pRKvrs

Mahakama kuu kanda ya Mwanza kesho inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi kupinga zuio la polisi kuuaga mwili wa aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Geita.https://youtu.be/kvCrIVoEYpk

Kesi inayowakabili wachina 4 wanaoshitakiwa kwa kuhujumu uchumi yaendelea jijini Mbeya huku shahidi wa kwanza akitoa ushahidi wake.https://youtu.be/m2PCOb7wPVE

Wananchi wakata ya Kambarage manispaa ya Shinyanga wamkamata muuguzi mkunga wa kituo cha afya cha Kambarage wakimtuhumu kuiba dawa za serikali.https://youtu.be/SWyN6aZ-DG4

Serikali kupitia ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma yasitisha ukodishaji wa kumbi kwa ajili ya kuendesha vikao pamoja na kutumia fedha kusafirisha watumishi wake. https://youtu.be/Mt995LPTKXM

Baadhi ya wananchi watoa maoni tofauti juu ya mvutano wa wabunge juu ya mkopo wa magari wa jumla ya shilingi milioni 90. https://youtu.be/gnOkB8BgylM

Katibu mkuu wa wizara ya afya awaagiza watendaji wote wa sekta ya afya kusimamia usafi kwenye maeneo yao ili kudhibiti uchafu unaosababisha magonjwa ya mlipuko kama vile Kipindupindu. https://youtu.be/89wkE5sj32g

No comments: