Sunday, December 4, 2016

DKT. SHEIN ATEMBELEA KIJIJI CHA MKONJONI KASKAZI UNGUJA, ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi alipowasili katika kijiji cha Mkonjoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja kuangalia ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kijijini hapo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Amali, Maalim Abdalla Mzee wakati alipotembelea Ujenzi wa Skuli mpya ya Sekondari katika Kijiji cha Mkonjoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja kuangalia ujenzi wa Skuli ya hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Vuai Mwinyi Mohamed wakiangalia kisima kiliopo katika kijiji cha Mkonjoni Wilaya ya Kaskazini B Unguja ambacho Wananchi wakijiji hicho hujipatia huduma ya maji kwa matatizo makubwa na usumbufu.
Vijana wa Kijiji cha Mkonjoni Jimbo la Kiwengwa ,Wilaya ya Kaskazini 'B' Mkoa wa Kaskazini Unguja walipokuwa wakimakaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) mara alipowasili Kijijini hapo akiwa katika ziara maalum mbapo pia alipata nafasi ya nkuzungumza nao.
Wananchi wa ​Kijiji cha Mkonjoni Jimbo la Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini 'B' Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na wananchi hao alipofanya ziara maalum ya kutembelea Kijiji hicho pia kuangalia Ujenzi wa Skuli Mpya inayojengwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi wa ​Kijiji cha Mkonjoni Jimbo la Kiwengwa Wilaya ya Kaskazini 'B' Mkoa wa Kaskazini Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea Kijiji hicho pia kuangalia Ujenzi wa Skuli Mpya inayojengwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Picha na Ikulu, Zanzibar.

No comments: