Sunday, December 4, 2016

RAIS WA ZANZIBAR DKT SHEIN ATEMBELEA MAJENGO MAPYA YA ZIMAMOTO UWANJA WA NDEGE

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kamishana wa Kikoso cha Zima Moto Zanzibar Abdalla Malimosi wakati alipokuwa akiaangalia picha za magari mapya ya kikosi hicho yanayotarajiwa kuwasili hivi karibuni,wakati alipotembelea ujenzi wa majengo mapya ya kikkosi hicho leo huko katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Wilaya ya Magharibi "A"Unguja
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar na Uongozi wa Kikosi cha Zima Moto na Uokozi, wakati alipofika kutembelea ujenzi wa majengo mapya ya kikosi hicho leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Zanzibar Abdulghani Himid Msoma wakati alipowasili katika Ofisi za Mamlaka hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea majengo mapya ya kikosi Zima Moto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi "A"Unguja leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi Mamlaka ya Viwanja wa Ndege Zanzibar na Uongozi wa Zima Moto na Uokozi  mara  alipowasili katika Ofisi za Mamlaka hiyo akiwa katika ziara ya kutembelea majengo mapya ya kikosi Zima Moto na Uokozi  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi "A"Unguja leo
 Jengo hili kama linavyoonekana baada ya kumalizika  Ujenzi wake  ambapo Kikosi cha Zimamoto na Uokozi   itakuwa ni Ofisi ya Kikosi hicho.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiangalia baadhi ya Vyumba vya Ofisi mpya ya Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi "A"Unguja leo,(wa pili kulia)Kamishna wa Kikosi hicho Abdalla Malimosi na SACF Simai Haji Simai
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiangalia Njia za kupitishia Umeme katika jengo jipya la Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume huko Kisauni Wilaya ya Magharibi "A"Unguja alipotembelea leo alipofanya ziara maalum
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Uongozi wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume alipotembelea kituo kidogo kinachofayiwa matengenezo akiwa katika ziara maalum leo,(kushoto)Kamishna wa Kikosi hicho Abdalla Malimosi na SACF Simai Haji Simai (wa pili kulia)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Abdalla Malimosi wakati  alipotembelea kituo kidogo kinachofayiwa matengenezo katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume   akiwa katika ziara maalum leo,(kushoto) Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mhe,Mohamed Ahmed Salum,(wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Haji Omar Kheri. Picha na Ikulu.

No comments: