Sunday, December 4, 2016

VIJANA WAHIMIZWA KUSHIRIKI MICHEZO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Hamad Massaun amewahimiza viajana nchini kushiriki michezo ili kuinua vipaji vitakavyowezesha Tanzania kupata wachezaji wazuri watakaoliwakilisha vyema taifa katika michezo ya kimataifa.

Massaun alitoa kauli hiyo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana ya jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park  ambacho kinahudumia vijana katika michezo mbalimbali.

Massaun alisema ikiwa wazazi watawasimamia vyema watoto wao katika michezo tangu wakiwa wadogo basi hapo baadaye nchi yetu itakuwa na wachezaji wengi ambao wataiwakilisha vyema nchi katika masdhindano mbalimbali.

“Katika nchi nyingine wachezaji wakubwa hawakuibukia ukubwani, walianza kujiimarisha tangu udogo wao na ndio maana wanafanya vizuri hivyo na sisi tujielekeze huko ili tuwe  na wachezaji bora kama wao na serikali itaendelea kutoa msaada wa kila aina unaohitajika ili kufanisha azma hiyo ” Alisema Massaun.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ufundi wa Kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park Bw. Ray Power alisema misaada itakayopatikana kutokana na michezo hiyo ya hisani itatumika kuwaendeleza vijana wadogo waliopo katika kituo hicho ambacho kimejumuisha michezo mbalimbali.

Katika kilele hicho Naibu Waziri Massaun alitoa zawadi mbalimbali kwa washindi katika michezo tofauti iliyoshirikishwa ikiwemo mpira wa miguu, tenesi, magongo na gofu. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akisalimiana na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST ya jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST (wenye jezi za blue) na timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy (wenye jezi nyeusi) kabla ya mchezo wao wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akimkabidhi kombe la ushindi nahodha wa timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy baada ya kuibuka mabigwa katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akikabidhiwa zawadi na Katibu wa Klabu ya Gymkhana ya jijini Dar es Salaam Khalal Rashid wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu hiyo jana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni akizungumza na Mkurugenzi wa ufundi wa kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam Bw. Ray Power wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe.Hamad Massauni (mwenye jezi nyekundu aliyesimama) akiwa katika picha ya pamoja na timu ya maveterani ya Gymkhana Dar es Salaam wakati alipokuwa mgeni rasmi katika michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana kwa ajili ya kuchangia kituo cha michezo Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa timu ya watoto kutoka shule ya IST, Jack Jere (kushoto) akijaribu kumtoka Mohamed Mchamungu wa timu ya watoto wa kituo cha Dar es Salaam Academy wakati wa michezo ya hisani iliyoandaliwa na klabu ya Gymkhana ikiwa na lengo la kusaidia kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Park cha jijini Dar es Salaam .(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi)

No comments: